Isa. 26:1-6 Swahili Union Version (SUV)

1. Siku ile wimbo huu utaimbwa katika nchi ya Yuda;Sisi tunao mji ulio na nguvu;Ataamuru wokovu kuwa kuta na maboma.

2. Wekeni wazi malango yake,Taifa lenye haki, lishikalo kweli, liingie.

3. Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemeaKatika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.

4. Mtumainini BWANA siku zoteMaana BWANA YEHOVA ni mwamba wa milele.

5. Kwa kuwa amewashusha wakaao juu,Mji ule ulioinuka, aushusha,Aushusha hata nchi, auleta hata mavumbini.

6. Mguu utaukanyaga chini,Naam, miguu yao walio maskini,Na hatua zao walio wahitaji.

Isa. 26