Isa. 22:1-9 Swahili Union Version (SUV)

1. Ufunuo juu ya bonde la maono.Sasa una nini, wewe,Hata umepanda pia juu ya dari za nyumba?

2. Ewe uliyejaa makelele,Mji wa ghasia, mji wenye furaha;Watu wako waliouawa hawakuuawa kwa upanga,Wala hawakufa vitani.

3. Wakuu wako wote wamekimbia pamoja,Wamefungwa wasiutumie upinde.Wote walioonekana wamefungwa pamoja,Wamekimbia mbali sana.

4. Kwa sababu hiyo nasema, Geuza uso wako usinitazame, nipate kulia kwa uchungu; usijishughulishe kunifariji, kwa ajili ya kuharibika kwake binti ya watu wangu.

5. Kwa maana siku ya kutaabika, siku ya kukanyagwa, siku ya fujo inakuja, itokayo kwa Bwana, BWANA wa majeshi, katika bonde la Maono; inabomoa kuta; na kuililia milima.

6. Na Elamu wameshika podo, pamoja na magari ya vita, na watu wenye kupanda farasi; na Kiri wameifunua ngao.

7. Hata ikawa mabonde yako mateule yamejaa magari ya vita, nao wapandao farasi wamejipanga wakielekea malango.

8. Kisha alikiondoa kifuniko cha Yuda, nawe siku hiyo ulivitazama vyombo vya vita katika nyumba ya mwituni.

9. Nanyi mlipaona mahali palipobomoka katika mji wa Daudi ya kuwa ni pengi, nanyi mliyakusanya maji ya birika la chini.

Isa. 22