10. Maana umemsahau Mungu wa wokovu wako, wala hukuukumbuka mwamba wa ngome yako; kwa sababu hiyo ulipanda mashamba yapendezayo, na kutia ndani yake mizabibu migeni.
11. Katika siku ile ulipopanda, ulifanya kitalu, na wakati wa asubuhi ulizimeesha mbegu zako, lakini mavuno yatatoweka siku ya huzuni, na ya sikitiko la moyo lifishalo.
12. Aha! Uvumi wa watu wengi!Wanavuma kama uvumi wa bahari;Aha! Ngurumo ya mataifa!Wananguruma kama ngurumo ya maji mengi;
13. Mataifa wananguruma kama ngurumo ya maji mengi;Lakini atawakemea, nao watakimbia mbali sana,Watafukuzwa kama makapi milimani mbele ya upepo,Na kama mavumbi vuruvuru mbele ya tufani.