1. Tia baragumu kinywani mwako. Kama tai, anakuja juu ya nyumba ya BWANA; kwa sababu wamelihalifu agano langu, wameiasi sheria yangu.
2. Watanililia, Mungu wangu, sisi Israeli tunakujua.
3. Israeli ameyatupa yaliyo mema; adui watamfuatia.
4. Wamesimamisha wafalme, lakini si kwa shauri langu; wamejifanyia wakuu, lakini nalikuwa sina habari; kwa fedha yao na dhahabu yao wamejifanyizia sanamu, kusudi wakatiliwe mbali.
5. Amemtupa ndama yako, Ee Samaria; hasira yangu imewaka juu yao; siku ngapi zitapita kabla ya hao kupata hali isiyo na hatia?
6. Maana katika Israeli kimetokea hata na kitu hiki; fundi ndiye aliyekifanya, nacho si mungu kamwe; naam, ndama ya Samaria itavunjika vipande vipande.
7. Kwa maana wao hupanda upepo, nao watavuna tufani; nafaka haina bua; machipuko yake hayatoi masuke; hata ikiwa yatoa, wageni watayameza.