1. Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
2. Nena na Haruni, ukamwambie, Utakapoziweka taa, hizo taa saba zitatoa nuru hapo mbele ya kinara cha taa.
3. Basi Haruni akafanya; akaziweka taa zake ili zitoe nuru hapo mbele ya kinara, kama BWANA alivyomwagiza Musa.
4. Na hii ndiyo kazi ya hicho kinara cha taa, ilikuwa ni kazi ya ufuzi wa dhahabu; tangu tako lake hata maua yake kilikuwa ni kazi ya ufuzi; vile vile kama ule mfano BWANA aliokuwa amemwonyesha Musa, ndivyo alivyokifanya kinara.
5. Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
6. Watwae Walawi na kuwaondoa kati ya wana wa Israeli, kisha uwatakase.
7. Nawe utawafanyia mambo haya ili kuwatakasa; nyunyiza juu yao maji yatakasayo dhambi, nao wajinyoe kwa wembe mwili wote, kisha wazifue nguo zao, na kujitakasa.
8. Kisha na watwae ng’ombe mume mmoja mchanga, na sadaka yake ya unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, nawe utatwaa ng’ombe mume mchanga mwingine kuwa sadaka ya dhambi.