Hes. 33:1-19 Swahili Union Version (SUV)

1. Hizi ndizo safari za wana wa Israeli, hapo walipotoka nchi ya Misri kwa jeshi zao chini ya mkono wa Musa na Haruni.

2. Musa akaandika jinsi walivyotoka katika safari zao, kwa amri ya BWANA; na hizi ndizo safari zao kama kutoka kwao kulivyokuwa.

3. Wakasafiri kutoka Ramesesi mwezi wa kwanza, siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza; siku ya pili baada ya Pasaka, wana wa Israeli wakatoka kwa mkono wa nguvu mbele ya macho ya Wamisri wote,

4. hapo Wamisri walipokuwa wanazika wazaliwa wa kwanza wao wote, BWANA aliokuwa amewapiga kati yao; BWANA akafanya hukumu juu ya miungu yao nayo.

5. Wana wa Israeli wakasafiri kutoka Ramesesi, wakapanga katika Sukothi.

6. Kisha wakasafiri kutoka Sukothi, wakapanga Ethamu, palipo katika mwisho wa nyika.

7. Wakasafiri kutoka Ethamu, na kurudi nyuma hata Pi-hahirothi palipokabili Baal-sefoni; wakapanga mbele ya Migdoli.

8. Wakasafiri kutoka hapo mbele ya Hahirothi, wakapita katikati ya bahari na kuingia jangwani; kisha wakaenda safari ya siku tatu katika nyika ya Ethamu, wakapanga Mara.

9. Wakasafiri kutoka Mara, wakafikilia Elimu; huko Elimu palikuwa na chemchemi za maji kumi na mbili, na mitende sabini; nao wakapanga hapo.

10. Wakasafiri kutoka Elimu wakapanga karibu na Bahari ya Shamu.

11. Wakasafiri kutoka Bahari ya Shamu, wakapanga katika nyika ya Sini.

12. Wakasafiri kutoka nyika ya Sini, wakapanga Dofka.

13. Wakasafiri kutoka Dofka, wakapanga Alushi.

14. Wakasafiri kutoka Alushi, wakapanga Refidimu, ambapo hapakuwa na maji ya watu kunywa.

15. Wakasafiri kutoka Refidimu, wakapanga katika nyika ya Sinai.

16. Wakasafiri kutoka nyika ya Sinai, wakapanga Kibroth-hataava.

17. Wakasafiri kutoka Kibroth-hataava, wakapanga Haserothi.

18. Wakasafiri kutoka Haserothi, wakapanga Rithma.

19. Wakasafiri kutoka Rithma, wakapanga Rimon-peresi.

Hes. 33