Hes. 31:29-42 Swahili Union Version (SUV)

29. twaa katika nusu yao, ukampe Eleazari kuhani, kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA.

30. Na katika hiyo nusu ya wana wa Israeli utatwaa mmoja atakayetolewa katika kila hamsini, katika wanadamu, na katika ng’ombe, na katika punda, na katika kondoo, maana, katika wanyama wote, ukawape Walawi, hao walindao ulinzi wa maskani ya BWANA.

31. Musa na Eleazari kuhani wakafanya kama BWANA alivyomwagiza Musa.

32. Basi masazo ya hizo nyara walizotwaa watu wa vita, zilikuwa ni kondoo mia sita na sabini na tano elfu,

33. na ng’ombe sabini na mbili elfu,

34. na punda sitini na moja elfu,

35. tena wanadamu jumla yao ilikuwa thelathini na mbili elfu, katika hao wanawake ambao hawakumjua mume kwa kulala pamoja naye.

36. Na hiyo nusu ambayo ilikuwa ni sehemu ya hao waliotoka kwenda vitani, hesabu yake ilikuwa kondoo mia tatu na thelathini na saba elfu na mia tano;

37. na kodi ya BWANA katika hao kondoo ilikuwa kondoo mia sita na sabini na watano.

38. Tena, ng’ombe walikuwa thelathini na sita elfu; na katika hao kodi ya BWANA ilikuwa ng’ombe sabini na wawili.

39. Na punda walikuwa thelathini elfuna mia tano, katika hao kodi ya BWANA ilikuwa punda sitini na mmoja.

40. Na wanadamu walikuwa watu kumi na sita elfu; katika hao sehemu ya BWANA ilikuwa ni watu thelathini na wawili.

41. Basi Musa akampa Eleazari kuhani hiyo sehemu, iliyokuwa sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA, kama BWANA alivyomwagiza Musa.

42. Tena katika hiyo nusu iliyokuwa ya wana wa Israeli, ambayo Musa aliitenga na watu waliokwenda vitani,

Hes. 31