42. Musa akahesabu, kama BWANA alivyomwagiza, wazaliwa wa kwanza wote katika wana wa Israeli.
43. Wazaliwa wa kwanza wote walio waume kwa hesabu ya majina, tangu umri wa mwezi mmoja na zaidi, katika hao waliohesabiwa kwao, walikuwa ishirini na mbili elfu na mia mbili na sabini na watatu.
44. Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
45. Uwatwae Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza katika wana wa Israeli, na wanyama wa Walawi badala ya wanyama wao; na hao Walawi watakuwa wangu mimi; mimi ndimi BWANA.
46. Tena kwa kuwakomboa hao watu mia mbili na sabini na watatu, wa hao wazaliwa wa kwanza wa Israeli, ambao wamezidi ile hesabu ya Walawi,
47. utatwaa shekeli tano kwa kichwa cha kila mtu kwa hiyo shekeli ya mahali patakatifu (shekeli ni gera ishirini);
48. na hizo fedha ambazo waliosalia wamekombolewa kwazo utampa Haruni na wanawe.
49. Basi Musa akawatoza fedha za ukombozi, hao waliozidi hesabu ya wale waliokombolewa na Walawi;
50. akatwaa hizo fedha kwa wazaliwa wa kwanza wa wana wa Israeli; shekeli elfu moja na mia tatu na sitini na tano kwa shekeli ya mahali patakatifu;
51. kisha hizo fedha za ukombozi Musa akampa Haruni na wanawe, kama neno la BWANA, kama BWANA alivyomwagiza Musa.