21. Hakutazama uovu katika Yakobo,Wala hakuona ukaidi katika Israeli.BWANA, Mungu wake, yu pamoja naye,Na sauti kuu ya mfalme i katikati yao.
22. Mungu amewaleta kutoka Misri,Naye ana nguvu kama nguvu za nyati.
23. Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo,Wala hapana uganga juu ya Israeli.Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa,Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!
24. Tazama, watu hawa wanaondoka kama simba mke,Na kama simba anajiinua nafsi yake,Hatalala hata atakapokula mawindo,Na kunywa damu yao waliouawa.
25. Balaki akamwambia Balaamu, Basi usiwalaani kabisa, wala usiwabariki kabisa.
26. Lakini Balaamu akajibu akamwambia Balaki, Je! Sikukuambia ya kwamba, Kila neno BWANA atakalolisema sina budi kulitenda?
27. Kisha Balaki akamwambia Balaamu, Haya, njoo sasa, nikupeleke mahali pengine; labda Mungu ataridhia kwamba unilaanie watu hao huko.
28. Basi Balaki akamchukua Balaamu akaenda naye mpaka kilele cha mlima Peori, mahali paelekeapo upande wa nyika iliyo chini yake.
29. Balaamu akamwambia Balaki, Haya, unijengee hapa madhabahu saba, kisha uniandalie ng’ombe waume saba, na kondoo waume saba.
30. Basi Balaki akafanya kama Balaamu alivyosema, akasongeza sadaka ng’ombe mume na kondoo mume juu ya kila madhabahu.