Hes. 23:1-8 Swahili Union Version (SUV)

1. Balaamu akamwambia Balaki, Nijengee hapa madhabahu saba, ukaniandalie hapa ng’ombe waume saba, na kondoo waume saba.

2. Balaki akafanya kama Balaamu alivyonena. Balaki na Balaamu wakatoa sadaka, ng’ombe mume mmoja na kondoo mume mmoja juu ya kila madhabahu.

3. Balaamu akamwambia Balaki, Simama karibu na sadaka yako, nami nitakwenda, labda BWANA atakuja kuonana nami; na lo lote atakalonionyesha nitakuambia. Akaenda hata mahali peupe juu ya kilima.

4. Mungu akakutana na Balaamu; naye Balaamu akamwambia, Nimetengeneza madhabahu saba, nami nimetoa sadaka ng’ombe mume mmoja na kondoo mume mmoja juu ya kila madhabahu.

5. BWANA akatia neno katika kinywa chake Balaamu, akasema, Umrudie Balaki; ukaseme maneno haya.

6. Akarudi kwake, na tazama, amesimama karibu na sadaka yake ya kuteketezwa, yeye na wakuu wote wa Moabu pamoja naye.

7. Akatunga mithali yake, akasema,Balaki amenileta kutoka Aramu,Mfalme wa Moabu kutoka milima ya mashariki,Njoo! Unilaanie Yakobo,Njoo! Unishutumie Israeli.

8. Nimlaanije, yeye ambaye Mungu hakumlaani?Nimshutumuje, yeye ambaye BWANA hakumshutumu?

Hes. 23