Mungu akakutana na Balaamu; naye Balaamu akamwambia, Nimetengeneza madhabahu saba, nami nimetoa sadaka ng’ombe mume mmoja na kondoo mume mmoja juu ya kila madhabahu.