8. Kwake nitanena mdomo kwa mdomo,Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo;Na umbo la BWANA yeye ataliona.Mbona basi ninyi hamkuogopaKumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?
9. Hasira za BWANA zikawaka juu yao; naye akaenda zake.
10. Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye ukoma.
11. Kisha Haruni akamwambia Musa, Ee bwana wangu nakusihi sana usituwekee dhambi juu yetu, kwa kuwa tumefanya ya upumbavu, na kufanya dhambi.
12. Nakusihi, asiwe kama mmoja aliyekufa, ambaye nyama ya mwili wake nusu imelika hapo atokapo tumbo la mama yake.
13. Musa akamlilia BWANA, akasema, Mpoze, Ee Mungu, nakusihi sana.
14. BWANA akamwambia Musa, Je! Kama baba yake angalimtemea mate usoni tu, hangaliona aibu muda wa siku saba? Na afungwe nje ya kambi muda wa siku saba, kisha baada ya hayo ataletwa ndani tena.
15. Basi Miriamu alifungwa nje ya kambi muda wa siku saba; wala watu hawakusafiri hata Miriamu alipoletwa ndani tena.
16. Baada ya hayo watu wakasafiri kutoka Haserothi, wakapanga kambi katika nyika ya Parani.