5. BWANA akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili.
6. Kisha akawaambia,Sikizeni basi maneno yangu;Akiwapo nabii kati yenu,Mimi, BWANA, nitajifunua kwake katika maono,Nitasema naye katika ndoto.
7. Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa;Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote;
8. Kwake nitanena mdomo kwa mdomo,Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo;Na umbo la BWANA yeye ataliona.Mbona basi ninyi hamkuogopaKumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?
9. Hasira za BWANA zikawaka juu yao; naye akaenda zake.