57. wana wa Shefatia, wana wa Hatili, wana wa Pokereth-Sebaimu, wana wa Amoni.
58. Wanethini wote, pamoja na watumwa wa Sulemani, walikuwa mia tatu tisini na wawili.
59. Na hawa ndio watu waliokwea kutoka Tel-mela, na Tel-harsha, na Kerubu, na Adani, na Imeri; walakini hawakuweza kuonyesha mbari za baba zao, wala kizazi chao, kwamba walikuwa wa Israeli;
60. wana wa Delaya, wana wa Tobia, wana wa Nekoda, mia sita hamsini na wawili.
61. Tena wa makuhani; wana wa Habaya, wana wa Hakosi, wana wa Barzilai, yule aliyeoa mmojawapo wa binti Barzilai, Mgileadi, akaitwa kwa jina lao.
62. Hao waliitafuta orodha yao miongoni mwa wale waliohesabiwa kwa nasaba, wasionekane; kwa hiyo walihesabiwa kuwa na unajisi.
63. Na huyo Tirshatha akawaambia kwamba wasile katika vitu vitakatifu sana, hata atakaposimama kuhani mwenye Urimu na Thumimu.
64. Basi hilo kusanyiko lote zima, jumla yake ilikuwa watu arobaini na mbili elfu na mia tatu na sitini,
65. tena, zaidi ya hao, kulikuwa na watumishi wao waume kwa wake, ambao walikuwa saba elfu, na mia tatu na thelathini na saba; nao walikuwa na waimbaji waume kwa wake mia mbili.
66. Farasi zao walikuwa mia saba thelathini na sita; nyumbu zao, mia mbili arobaini na watano;
67. ngamia zao, mia nne thelathini na watano; punda zao elfu sita, na mia saba na ishirini.