Ayu. 8:8-16 Swahili Union Version (SUV)

8. Basi, uwaulize, tafadhali, vizazi vya zamani,Ujitie kuyaangalia yale baba zao waliyoyatafuta;

9. (Kwani sisi tu wa jana tu, wala hatujui neno,Kwa kuwa siku zetu duniani ni kivuli tu;)

10. Je! Hawatakufunza wao, na kukueleza,Na kutamka maneno yatokayo mioyoni mwao?

11. Je! Hayo mafunjo yamea pasipo matopeNa makangaga kumea pasipo maji?

12. Yakiwa yakali mabichi bado, wala hayakukatwa,Hunyauka mbele ya majani mengine.

13. Ndivyo ulivyo mwisho wa hao wamsahauo Mungu;Na matumaini yake huyo mbaya huangamia;

14. Uthabiti wake utavunjika,Na matumaini yake huwa ni nyuzi za buibui.

15. Ataitegemea nyumba yake, isisimame;Atashikamana nayo, isidumu.

16. Yeye huwa mti mbichi mbele ya jua,Nayo machipukizi yake huenea katika bustani yake.

Ayu. 8