Ayu. 8:4-12 Swahili Union Version (SUV)

4. Kwamba watoto wako wamemfanyia dhambi,Naye amewatia mkononi mwa kosa lao;

5. Wewe ukimtafuta Mungu kwa bidii,Na kumsihi huyo Mwenyezi;

6. Ukiwa wewe u safi na mwelekevu;Hakika yeye sasa angeamka kwa ajili yako,Na kuyafanya makazi ya haki yako kufanikiwa.

7. Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo,Lakini mwisho wako ungeongezeka sana.

8. Basi, uwaulize, tafadhali, vizazi vya zamani,Ujitie kuyaangalia yale baba zao waliyoyatafuta;

9. (Kwani sisi tu wa jana tu, wala hatujui neno,Kwa kuwa siku zetu duniani ni kivuli tu;)

10. Je! Hawatakufunza wao, na kukueleza,Na kutamka maneno yatokayo mioyoni mwao?

11. Je! Hayo mafunjo yamea pasipo matopeNa makangaga kumea pasipo maji?

12. Yakiwa yakali mabichi bado, wala hayakukatwa,Hunyauka mbele ya majani mengine.

Ayu. 8