Ayu. 8:17-22 Swahili Union Version (SUV)

17. Mizizi yake huzonga-zonga chuguu,Huangalia mahali penye mawe.

18. Lakini, aking’olewa mahali pake,Ndipo patamkana, na kusema, Mimi sikukuona.

19. Tazama, furaha ya njia yake ni hii,Na wengine watachipuka kutoka katika nchi.

20. Tazama, Mungu hatamtupa mtu mkamilifu,Wala hatawathibitisha watendao uovu.

21. Bado atakijaza kinywa chako kicheko,Na midomo yako ataijaza shangwe.

22. Hao wakuchukiao watavikwa aibu;Nayo hema yake mwovu haitakuwako tena.

Ayu. 8