13. Ndivyo ulivyo mwisho wa hao wamsahauo Mungu;Na matumaini yake huyo mbaya huangamia;
14. Uthabiti wake utavunjika,Na matumaini yake huwa ni nyuzi za buibui.
15. Ataitegemea nyumba yake, isisimame;Atashikamana nayo, isidumu.
16. Yeye huwa mti mbichi mbele ya jua,Nayo machipukizi yake huenea katika bustani yake.
17. Mizizi yake huzonga-zonga chuguu,Huangalia mahali penye mawe.
18. Lakini, aking’olewa mahali pake,Ndipo patamkana, na kusema, Mimi sikukuona.