1. Ndipo Bildadi huyo Mshuhi akajibu, na kusema,
2. Wewe utanena maneno haya hata lini?Maneno ya kinywa chako yatakuwa kama upepo mkuu hata lini?
3. Je! Mungu hupotosha hukumu?Au, huyo Mwenyezi hupotosha yaliyo ya haki?
4. Kwamba watoto wako wamemfanyia dhambi,Naye amewatia mkononi mwa kosa lao;
5. Wewe ukimtafuta Mungu kwa bidii,Na kumsihi huyo Mwenyezi;