Ayu. 7:13-21 Swahili Union Version (SUV)

13. Hapo nisemapo, kitanda changu kitanituza moyo,Malazi yangu yatanipunguzia kuugua kwangu;

14. Ndipo unitishapo kwa ndoto,Na kunitia hofu kwa maono;

15. Hata nafsi yangu huchagua kunyongwa,Na kuchagua kifo kuliko maumivu yangu haya.

16. Ninadhoofika; sitaishi sikuzote;Usinisumbue, kwani siku zangu ni uvuvio.

17. Je! Mtu ni kitu gani, hata ukamtukuza,Na kumtia moyoni mwako,

18. Na kumwangalia kila asubuhi,Na kumjaribu kila dakika?

19. Je! Hata lini hukomi kuniangalia;Wala kunisumbua hata nimeze mate?

20. Kwamba nimefanya dhambi, nikufanyieje Ee mlinda wanadamu?Mbona umeniweka niwe shabaha yako,Hata nimekuwa mzigo kwa nafsi yangu?

21. Nawe, je! Mbona hunisamehe makosa yangu,Na kuniondolea maovu yangu?Kwa kuwa sasa nitalala mavumbini;Nawe utanitafuta kwa bidii, lakini sitakuwapo.

Ayu. 7