Ayu. 39:23-30 Swahili Union Version (SUV)

23. Podo humpigia makelele,Mkuki ung’aao na fumo.

24. Huimeza nchi kwa ukali wake na ghadhabu;Wala hasimami kwa sauti ya baragumu.

25. Kila ipigwapo baragumu yeye husema, Aha!Naye husikia harufu ya vita toka mbali,Mshindo wa maakida, na makelele.

26. Je! Mwewe huruka juu kwa akili zako,Na kuyanyosha mabawa yake kwenda kusini?

27. Je! Tai hupaa juu kwa amri yako,Na kufanya kioto chake mahali pa juu?

28. Hukaa jabalini, ndiko kwenye malazi yake,Juu ya genge la jabali, na ngomeni.

29. Toka huko yeye huchungulia mawindo;Macho yake huyaangalia toka mbali.

30. Makinda yake nayo hufyonza damu;Na kwenye maiti ndiko aliko.

Ayu. 39