1. Je! Wajua majira ya kuzaa kwao mbuzi-mwitu walio majabalini?Au waweza kusema majira ya kuzaa kulungu?
2. Je! Waweza kuhesabu miezi yao watakayoitimiza?Au je! Wajua majira ya kuzaa kwao?
3. Wao hujiinamisha, kuzaa watoto wao,Watupa taabu zao.
4. Watoto wao wa katika hali nzuri, hukua katika bara wazi;Huenda zao, wala hawarudi tena.
5. Ni nani aliyempeleka punda-milia aende huru?Au je! Ni nani aliyemfungulia vifungo punda-mwitu?