Ayu. 38:6-14 Swahili Union Version (SUV)

6. Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani?Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni,

7. Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja,Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?

8. Au ni nani aliyeifunga bahari kwa milango,Hapo ilipofurika kana kwamba imetoka tumboni.

9. Nilipolifanya wingu kuwa vazi lake,Na giza zito kuwa nguo ya kuifungia,

10. Nikaiagiza amri yangu;Nikaiwekea makomeo na milango,

11. Nikasema, Utafika mpaka hapa, lakini hutapita,Na hapa mawimbi yako yanyetayo yatazuiliwa?

12. Je! Umeiamuru asubuhi tangu siku zako zilipoanza?Umeyajulisha mapambazuko mahali pake?

13. Yapate kuishika miisho ya nchi,Waovu wakung’utwe wakawe mbali nayo?

14. Hubadilika mfano wa udongo chini ya muhuri,Vitu vyote vinatokea kama mavazi.

Ayu. 38