Ayu. 38:5-21 Swahili Union Version (SUV)

5. Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake, kama ukijua?Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake?

6. Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani?Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni,

7. Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja,Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?

8. Au ni nani aliyeifunga bahari kwa milango,Hapo ilipofurika kana kwamba imetoka tumboni.

9. Nilipolifanya wingu kuwa vazi lake,Na giza zito kuwa nguo ya kuifungia,

10. Nikaiagiza amri yangu;Nikaiwekea makomeo na milango,

11. Nikasema, Utafika mpaka hapa, lakini hutapita,Na hapa mawimbi yako yanyetayo yatazuiliwa?

12. Je! Umeiamuru asubuhi tangu siku zako zilipoanza?Umeyajulisha mapambazuko mahali pake?

13. Yapate kuishika miisho ya nchi,Waovu wakung’utwe wakawe mbali nayo?

14. Hubadilika mfano wa udongo chini ya muhuri,Vitu vyote vinatokea kama mavazi.

15. Na waovu nuru yao huzuiliwa isiwafikie,Na mkono ulioinuka huvunjika.

16. Je! Umeziingia chemchemi za bahari,Au umetembea mahali pa siri pa vilindi?

17. Je! Umefunuliwa malango ya mauti,Au umeyaona malango ya kuzimu?

18. Umeyafahamu mapana ya dunia?Haya! Sema, ikiwa unayajua hayo yote.

19. Iko wapi njia ya kuyafikia makao ya nuru?Na giza pia, mahali pake ni wapi?

20. Upate kuipeleka hata mpaka wake,Upate kuelewa na mapito ya kuiendea nyumba yake?

21. Hukosi unajua, maana ulizaliwa wakati huo,Na hesabu ya siku zako ni kubwa!

Ayu. 38