Ayu. 38:35-41 Swahili Union Version (SUV)

35. Waweza kuutuma umeme, nao ukaenda,Ukakuambia, Sisi tupo hapa?

36. Je! Ni nani aliyetia hekima moyoni?Au ni nani aliyetia ufahamu rohoni?

37. Ni nani awezaye kuyahesabu mawingu kwa hekima?Au ni nani awezaye kuzimimina chupa za mbinguni?

38. Wakati mavumbi yagandamanapo,Na madongoa kushikamana pamoja?

39. Je! Utamwindia simba mke mawindo?Au utashibisha njaa ya simba wachanga,

40. Waoteapo mapangoni mwao,Wakaapo mafichoni wapate kuvizia?

41. Ni nani anayempatia kunguru chakula,Makinda yake wanapomlilia Mungu,Na kutanga-tanga kwa kutindikiwa na chakula?

Ayu. 38