3. Basi jifunge viuno kama mwanamume,Maana nitakuuliza neno, nawe niambie.
4. Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi?Haya! Sema, kama ukiwa na ufahamu.
5. Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake, kama ukijua?Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake?
6. Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani?Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni,
7. Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja,Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?
8. Au ni nani aliyeifunga bahari kwa milango,Hapo ilipofurika kana kwamba imetoka tumboni.