29. Barafu ilitoka katika tumbo la nani?Na sakitu ya mbinguni ni nani aliyeizaa?
30. Maji hugandamana kama jiwe,Na uso wa vilindi huganda kwa baridi.
31. Je! Waweza kuufunga mnyororo wa Kilimia,Au kuvilegeza vifungo vya Orioni?
32. Je! Waweza kuziongoza Sayari kwa wakati wake?Au waweza kuongoza Dubu na watoto wake?
33. Je! Unazijua amri zilizoamuriwa mbingu?Waweza kuyathibitisha mamlaka yake juu ya dunia?
34. Waweza kuiinua sauti yako mpaka mawinguni,ili wingi wa maji ukufunikize?
35. Waweza kuutuma umeme, nao ukaenda,Ukakuambia, Sisi tupo hapa?
36. Je! Ni nani aliyetia hekima moyoni?Au ni nani aliyetia ufahamu rohoni?