Ayu. 33:21-27 Swahili Union Version (SUV)

21. Nyama ya mwili wake huliwa, isionekane;Na mifupa yake isiyoonekana yatokea nje.

22. Naam, nafsi yake inakaribia shimoni,Na uhai wake unakaribia waangamizi.

23. Kwamba akiwapo malaika pamoja naye,Mkalimani, mmoja katika elfu,Ili kumwonyesha binadamu hayo yampasayo;

24. Ndipo amwoneapo rehema, na kusema,Mwokoe asishuke shimoni;Mimi nimeuona ukombozi.

25. Nyama ya mwili wake itakuwa laini kuliko ya mtoto;Huzirudia siku za ujana wake;

26. Yeye humwomba Mungu, naye akamtakabalia;Hata auone uso wake kwa furaha;Naye humrejezea mtu haki yake.

27. Yeye huimba mbele ya watu, na kusema,Mimi nimefanya dhambi, na kuyapotosha hayo yaliyoelekea,Wala sikulipizwa jambo hilo;

Ayu. 33