Ayu. 33:18-29 Swahili Union Version (SUV)

18. Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni,Na uhai wake usiangamie kwa upanga.

19. Yeye hutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake,Na kwa mashindano yaendeleayo daima mifupani mwake;

20. Hata roho yake huchukia chakula,Na nafsi yake huchukia nyama nzuri.

21. Nyama ya mwili wake huliwa, isionekane;Na mifupa yake isiyoonekana yatokea nje.

22. Naam, nafsi yake inakaribia shimoni,Na uhai wake unakaribia waangamizi.

23. Kwamba akiwapo malaika pamoja naye,Mkalimani, mmoja katika elfu,Ili kumwonyesha binadamu hayo yampasayo;

24. Ndipo amwoneapo rehema, na kusema,Mwokoe asishuke shimoni;Mimi nimeuona ukombozi.

25. Nyama ya mwili wake itakuwa laini kuliko ya mtoto;Huzirudia siku za ujana wake;

26. Yeye humwomba Mungu, naye akamtakabalia;Hata auone uso wake kwa furaha;Naye humrejezea mtu haki yake.

27. Yeye huimba mbele ya watu, na kusema,Mimi nimefanya dhambi, na kuyapotosha hayo yaliyoelekea,Wala sikulipizwa jambo hilo;

28. Yeye ameikomboa nafsi yangu isiende shimoni,Na uhai wangu utautazama mwanga.

29. Tazama, hayo yote ni Mungu anayeyafanya,Mara mbili, naam, hata mara tatu, kwa mtu,

Ayu. 33