Ayu. 32:1-9 Swahili Union Version (SUV)

1. Basi hao watu watatu wakaacha kumjibu Ayubu, kwa sababu alikuwa mwenye haki machoni pake mwenyewe.

2. Ndipo zikawaka hasira za huyo Elihu mwana wa Barakeli, Mbuzi, katika jamaa ya Ramu, juu ya Ayubu, kwa sababu alikuwa amejipa haki mwenyewe zaidi ya Mungu.

3. Tena hasira zake ziliwaka juu ya hao rafiki zake watatu kwa sababu hawakupata jawabu, lakini wamemhukumia Ayubu makosa.

4. Basi huyo Elihu alikuwa anangoja ili anene na Ayubu, kwa sababu hao wengine walikuwa wazee kuliko yeye.

5. Hata Elihu alipoona kuwa hapana jawabu katika vinywa vya watu hao watatu, hasira zake ziliwaka.

6. Basi Elihu mwana wa Barakeli, Mbuzi, akajibu, na kusema,Mimi ni kijana, na ninyi ni wazee sana;Kwa hiyo nilijizuia, nisithubutu kuwaonyesha nionavyo.

7. Nilisema, Yafaa siku ziseme,Na wingi wa miaka ufundishe hekima.

8. Lakini imo roho ndani ya mwanadamu,Na pumzi za Mwenyezi huwapa akili.

9. Sio wakuu walio wenye akili,Wala sio wazee watambuao hukumu.

Ayu. 32