Ayu. 30:1-3 Swahili Union Version (SUV)

1. Lakini sasa hao walio wadogo wangu hunifanyia mzaha,Ambao baba zao niliwadharau hata kuwaweka na mbwa wa kundi langu.

2. Naam, uwezo wa mikono yao utanifaa nini?Watu ambao nguvu zao zimekoma.

3. Wamekonda kwa uhitaji na njaa;Huguguna nchi kavu, penye giza la ukiwa na uharibifu.

Ayu. 30