Ayu. 29:8-17 Swahili Union Version (SUV)

8. Hao vijana waliniona wakajificha,Nao wazee wakaniondokea na kusimama;

9. Wakuu wakanyamaa wasinene,Na kuweka mikono yao vinywani mwao;

10. Sauti yao masheki ilinyamaa,Na ndimi zao zilishikamana na makaakaa yao.

11. Maana sikio liliponisikia, ndipo likanibarikia;Na jicho liliponiona, likanishuhudia.

12. Kwa sababu nalimwokoa maskini aliyenililia;Yatima naye, na yule asiyekuwa na mtu wa kumsaidia.

13. Baraka yake yeye aliyekuwa karibu na kupotea ilinijia;Nikaufanya moyo wa mjane kuimba kwa furaha.

14. Nalijivika haki, ikanifunika,Adili yangu ilikuwa kama joho na kilemba.

15. Nalikuwa macho kwa kipofu,Nalikuwa miguu kwa aliyechechemea.

16. Nalikuwa baba kwa mhitaji,Na daawa ya mtu nisiyemjua naliichunguza.

17. Nami nilizivunja taya za wasio haki,Na kumpokonya mawindo katika meno yake.

Ayu. 29