20. Utukufu wangu utakuwa mpya kwangu,Na uta wangu hurejezwa upya mkononi mwangu.
21. Watu walitega masikio kunisikiliza, na kungoja,Wakanyamaa kimya wapate sikia mashauri yangu.
22. Hawakunena tena baada ya kusikia maneno yangu;Matamko yangu yakadondoka juu yao.
23. Walikuwa wakiningojea kama kungojea mvua;Wakafunua vinywa vyao sana kama mvua ya masika.
24. Walipokata tamaa nikacheka nao;Na mwanga wa uso wangu hawakuuangusha.
25. Niliwachagulia njia, nikakaa kama mkuu wao.Nikakaa kama mfalme katika jeshi la askari,Mfano wa awafarijiye hao waombolezao.