18. Ndipo niliposema, Nitakufa ndani ya kioto changu,Nami nitaziongeza siku zangu kama mchanga;
19. Shina langu limeenea hata kufika majini,Na umande hukaa usiku kucha katika matawi yangu;
20. Utukufu wangu utakuwa mpya kwangu,Na uta wangu hurejezwa upya mkononi mwangu.