1. Kisha Ayubu akaendelea na mithali yake, na kusema,
2. Laiti ningekuwa kama nilivyokuwa katika miezi ya kale,Kama katika siku hizo Mungu aliponilinda;
3. Hapo taa yake ilipomulika juu yangu kichwani,Nami nilitembea gizani kwa njia ya mwanga wake;
4. Kama nilivyokuwa katika siku zangu za kukomaa,Hapo siri ya Mungu ilipokuwa hemani mwangu;
5. Wakati Mwenyezi alipokuwa akali pamoja nami,Nao watoto wangu walipokuwa wakinizunguka;
6. Wakati hatua zangu zilipokuwa zikioshwa kwa siagi,Nalo jabali liliponimiminia mito ya mafuta!
7. Wakati nilipotoka kwenda mjini, hata langoni,Nilipokitengeza kiti changu katika njia kuu,