8. Wanyama wakali wajivunao hawajaikanyaga,Wala simba mkali hajaipita.
9. Huunyoshea mwamba wa gumegume mkono wake;Huipindua milima hata misingi yake.
10. Hukata mifereji kati ya majabali;Na jicho lake huona kila kito cha thamani
11. Hufunga vijito visichuruzike;Na kitu kilichostirika hukifunua.
12. Bali hekima itapatikana wapi?Na mahali pa ufahamu ni wapi?
13. Mwanadamu hajui thamani yake,Wala haionekani katika nchi ya walio hai.
14. Vilindi vyasema, Haimo ndani yangu;Na bahari yasema, Haiko kwangu.
15. Haipatikani kwa dhahabu,Wala fedha haitapimwa iwe thamani yake.
16. Haiwezi kutiwa thamani kwa dhahabu ya Ofiri,Wala kwa shohamu ya thamani nyingi, wala kwa yakuti ya samawi.
17. Dhahabu na vioo haviwezi kulinganishwa nayo;Wala kubadili kwake hakutakuwa kwa vyombo vya dhahabu safi.
18. Havitatajwa fedhaluka wala bilauri;Naam, kima cha hekima chapita marijani.
19. Yakuti ya rangi ya manjano ya Kushi haitasawazishwa nayo,Wala haitatiwa kima kwa dhahabu safi.