1. Kisha Ayubu akaendelea na mithali yake, na kusema,
2. Kama aishivyo Mungu, aliyeniondolea haki yangu;Huyo Mwenyezi aliyeitesa nafsi yangu;
3. (Kwa kuwa uhai wangu ukali mzima ndani yangu,Na roho ya Mungu i katika pua yangu;)
4. Hakika midomo yangu haitanena yasiyo haki,Wala ulimi wangu hautatamka udanganyifu.
5. Hasha! Nisiwahesabie ninyi kuwa na haki;Hata nitakapokufa sitajiondolea uelekevu wangu.
6. Haki yangu naishika sana, wala sitaiacha;Moyo wangu hautanisuta wakati nikiwapo hai.
7. Adui yangu na awe kama huyo mwovu,Na mwenye kuondoka kinyume changu na awe kama asiye haki.
8. Kwani tumaini la mpotovu ni nini, ingawa ajipatia faida,Hapo Mungu amwondoleapo roho yake?