Ayu. 27:1-7 Swahili Union Version (SUV)

1. Kisha Ayubu akaendelea na mithali yake, na kusema,

2. Kama aishivyo Mungu, aliyeniondolea haki yangu;Huyo Mwenyezi aliyeitesa nafsi yangu;

3. (Kwa kuwa uhai wangu ukali mzima ndani yangu,Na roho ya Mungu i katika pua yangu;)

4. Hakika midomo yangu haitanena yasiyo haki,Wala ulimi wangu hautatamka udanganyifu.

5. Hasha! Nisiwahesabie ninyi kuwa na haki;Hata nitakapokufa sitajiondolea uelekevu wangu.

6. Haki yangu naishika sana, wala sitaiacha;Moyo wangu hautanisuta wakati nikiwapo hai.

7. Adui yangu na awe kama huyo mwovu,Na mwenye kuondoka kinyume changu na awe kama asiye haki.

Ayu. 27