11. Nguzo za mbingu zatetemeka,Na kustaajabu kwa kukemea kwake.
12. Huichafua bahari kwa uwezo wake,Na kumtema Rahabu kwa akili zake.
13. Hizo mbingu hupambwa kwa roho yake;Mkono wake umemchoma nyoka aendaye mbio.
14. Tazama, hivi ni viunga tu vya njia zake;Na jinsi yalivyo madogo manong’ono tusikiayo katika habari zake!Lakini ngurumo za uweza wake ni nani awezaye kuelewa nazo?