Ayu. 20:26-29 Swahili Union Version (SUV)

26. Giza lote linawekwa kwa ajili ya hazina zake;Moto ambao haukuvuviwa na mtu utamla;Utayateketeza yaliyosalia hemani mwake.

27. Mbingu zitafunua wazi uovu wake,Nayo nchi itainuka kinyume chake.

28. Maongeo ya nyumba yake yataondoka,Yatamwagika mbali katika siku ya ghadhabu zake.

29. Hii ndiyo sehemu ya mtu mwovu itokayo kwa Mungu,Na urithi aliowekewa na Mungu.

Ayu. 20