Ayu. 19:17-29 Swahili Union Version (SUV)

17. Pumzi zangu ni kama za mgeni kwa mke wangu,Nami ni machukizo kwa ndugu zangu.

18. Hata watoto wadogo hunidharau;Nikiondoka, huninena.

19. Wasiri wangu wote wanichukia;Na hao niliowapenda wamenigeukia.

20. Mfupa wangu unagandamana na ngozi yangu na nyama yangu,Nami nimeokoka na ngozi ya meno yangu tu.

21. Nihurumieni, nihurumieni, enyi rafiki zangu,Kwa maana mkono wa Mungu umenigusa.

22. Mbona ninyi mnaniudhi kama Mungu,Wala hamkutosheka na nyama yangu?

23. Laiti maneno yangu yangeandikwa sasa!Laiti yangeandikwa kitabuni!

24. Yakachorwa katika mwamba milele,Kwa kalamu ya chuma na risasi.

25. Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai,Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi.

26. Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi,Lakini, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mungu;

27. Nami nitamwona mimi nafsi yangu,Na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine.Mtima wangu unazimia ndani yangu!

28. Kama mkisema, Jinsi tutakavyomwudhi!Kwa kuwa shina la jambo hili limeonekana kwake;

29. Uogopeni upanga;Kwa maana adhabu za upanga zina ghadhabu,Mpate kujua ya kwamba hukumu iko.

Ayu. 19