Ayu. 16:1-10 Swahili Union Version (SUV)

1. Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,

2. Nimesikia maneno mengi mfano wa hayo;Ninyi nyote ni wafariji wenye kutaabisha.

3. Je! Maneno yasiyo faida yatakuwa na mwisho?Au, kuna nini kinachokukasirisha, hata ukajibu?

4. Mimi nami ningeweza kunena kama ninyi;Kama roho zenu zingekuwa mahali pa roho yangu,Ningeweza kutunga maneno juu yenu,Na kuwatikisia ninyi kichwa changu.

5. Lakini ningewatia nguvu kwa kinywa changu,Na utuzo wa midomo yangu ungetuliza.

6. Nijapokuwa nanena, huzuni yangu haitulizwi;Nijapokuwa najizuia, nimepunguziwa kitu gani?

7. Lakini sasa amenichokesha;Jamii yangu yote umeifanya ukiwa.

8. Umenishika sana, ni ushahidi juu yangu;Na kukonda kwangu kwaniinukia, kwanishuhudia usoni pangu.

9. Amenirarua katika ghadhabu zake, na kunionea;Amesaga-saga meno juu yangu;Mtesi wangu hunikazia macho makali.

10. Wamenifumbulia vinywa vyao;Wamenipiga shavuni kwa kunitukana;Hujikutanisha pamoja juu yangu.

Ayu. 16