Ayu. 12:8-11 Swahili Union Version (SUV)

8. Au nena na nchi, nayo itakufundisha;Nao samaki wa baharini watakutangazia.

9. Katika hawa wote ni yupi asiyejua,Kwamba ni mkono wa BWANA uliofanya haya?

10. Ambaye nafsi ya kila kilicho hai i mkononi mwake,Na pumzi zao wanadamu wote.

11. Je! Sikio silo lijaribulo maneno,Kama vile kaakaa lionjavyo chakula?

Ayu. 12