15. Tazama, yuayazuia maji, nayo yakatika;Tena, huyapeleka, nayo yaipindua dunia.
16. Kwake yeye ziko nguvu, na makusudi kufanikiwa;Huyo adanganywaye, na mdanganyi pia ni wake.
17. Yeye huwaondoa washauri hali wametekwa nyara,Naye huwafanya waamuzi kuwa ni wapumbavu.
18. Yeye hulegeza kifungo cha wafalme,Na kuwafunga viuno vyao kwa mshipi.
19. Yeye huwaondoa makuhani hali wametekwa nyara.Na kuwapindua mashujaa.
20. Huondoa matamko ya hao walioaminiwa,Na kuondoa fahamu za wazee.
21. Humwaga aibu juu ya hao wakuu,Na kulegeza mshipi wa wenye nguvu.
22. Huvumbua mambo ya siri tokea gizani,Na hicho kilicho giza tupu huleta mwangani.
23. Huyaongeza mataifa, na kuyaangamiza;Huyaeneza mataifa mbali, na kuyaacha.