10. Yeye akipita, na kufunga watu,Na kuwaita hukumuni, ni nani basi awezaye kumzuia?
11. Kwani yeye awajua watu baradhuli;Huona na uovu pia, hata asipoufikiri.
12. Lakini mpumbavu aweza kupata ufahamu,Ingawa mwanadamu huzaliwa kama mtoto wa punda-mwitu.
13. Wewe ukiuweka moyo wako kwa uelekevu,Na kumnyoshea mikono yako;
14. Ikiwa una uovu mkononi mwako, uweke mbali nawe,Wala usikubali upuzi kukaa hemani mwako;
15. Hakika ndipo utakapopata kuinua uso pasipo ila;Naam, utathibitika, wala hutakuwa na hofu;
16. Kwa kuwa utasahau mashaka yako;Utayakumbuka kama maji yaliyokwisha pita;
17. Na maisha yako yatakuwa meupe kuliko adhuhuri;Lijapokuwa ni giza, litakuwa kama alfajiri.
18. Nawe utakuwa salama, kwa sababu kuna matumaini;Naam, utatafuta-tafuta kando yako, na kupumzika katika salama.
19. Tena utalala, wala hapana atakayekutia hofu;Naam, wengi watakutafuta uso wako.
20. Lakini macho ya waovu yataingia kiwi,Nao hawatakuwa na njia ya kukimbilia,Na matumaini yao yatakuwa ni kutoa roho.