2 Sam. 22:3-11 Swahili Union Version (SUV)

3. Mungu wa mwamba wangu, nitamwamini yeye;Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, mnara wangu, namakimbilio yangu;Mwokozi wangu, waniokoa na jeuri.

4. Nitamwita BWANA astahiliye kusifiwa;Hivyo nitaokoka na adui zangu.

5. Maana mawimbi ya mauti yalinizunguka,Mafuriko ya uovu yakanitia hofu.

6. Kamba za kuzimu zilinizunguka;Mitego ya mauti ikanikabili.

7. Katika shida yangu nalimwita BWANA,Naam, nikamlalamikia Mungu wangu;Naye akaisikia sauti yangu hekaluni mwake,Kilio changu kikaingia masikioni mwake.

8. Ndipo nchi ilipotikisika na kutetemeka,Misingi ya mbinguni ikasuka-sukaNa kutikisika, kwa sababu alikuwa na ghadhabu.

9. Kukapanda moshi kutoka puani mwake,Moto ukatoka kinywani mwake ukala;Makaa yakawashwa nao.

10. Aliziinamisha mbingu akashuka;Kukawa na giza kuu chini ya miguu yake.

11. Akapanda juu ya kerubi akaruka;Naam, alionekana juu ya mabawa ya upepo.

2 Sam. 22