1. Basi Daudi akamwambia BWANA maneno ya wimbo huu, siku ile BWANA alipomwokoa mikononi mwa adui zake zote, na mkononi mwa Sauli;
2. akasema,BWANA ndiye jabali langu, na ngome yangu, na mwokozi wangu,naam, wangu;
3. Mungu wa mwamba wangu, nitamwamini yeye;Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, mnara wangu, namakimbilio yangu;Mwokozi wangu, waniokoa na jeuri.
4. Nitamwita BWANA astahiliye kusifiwa;Hivyo nitaokoka na adui zangu.
5. Maana mawimbi ya mauti yalinizunguka,Mafuriko ya uovu yakanitia hofu.
6. Kamba za kuzimu zilinizunguka;Mitego ya mauti ikanikabili.
7. Katika shida yangu nalimwita BWANA,Naam, nikamlalamikia Mungu wangu;Naye akaisikia sauti yangu hekaluni mwake,Kilio changu kikaingia masikioni mwake.
8. Ndipo nchi ilipotikisika na kutetemeka,Misingi ya mbinguni ikasuka-sukaNa kutikisika, kwa sababu alikuwa na ghadhabu.
9. Kukapanda moshi kutoka puani mwake,Moto ukatoka kinywani mwake ukala;Makaa yakawashwa nao.
10. Aliziinamisha mbingu akashuka;Kukawa na giza kuu chini ya miguu yake.