2 Nya. 12:14-16 Swahili Union Version (SUV)

14. Naye akatenda yaliyo maovu, kwa kuwa hakuukaza moyo wake amtafute BWANA.

15. Basi mambo yake Rehoboamu, ya kwanza na ya mwisho, je! Hayakuandikwa katika tarehe za Shemaya nabii na Ido mwonaji, kwa jinsi ya kuandika nasaba? Kulikuwa na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu siku zote.

16. Rehoboamu akalala na babaze, akazikwa katika mji wa Daudi. Na Abiya mwanawe alitawala mahali pake.

2 Nya. 12