2 Nya. 11:2-15 Swahili Union Version (SUV)

2. Lakini neno la BWANA likamjia Shemaya mtu wa Mungu, kusema,

3. Mwambie Rehoboamu mwana wa Sulemani, mfalme wa Yuda, uwaambie na Israeli wote waliomo Yuda na Benyamini, ukisema,

4. BWANA asema hivi, Hamtapanda wala kupigana na ndugu zenu; rudini kila mtu nyumbani kwake; kwa kuwa jambo hili limetoka kwangu. Basi, wakayasikiliza maneno ya BWANA, wakarudi katika kumwendea Yeroboamu.

5. Naye Rehoboamu akakaa Yerusalemu, akajenga miji yenye ngome katika Yuda.

6. Akajenga na Bethlehemu, na Etamu, na Tekoa,

7. na Bethsuri, na Soko, na Adulamu,

8. na Gathi, na Maresha, na Zifu,

9. na Adoraimu, na Lakishi, na Azeka,

10. na Sora, na Aiyaloni, na Hebroni, iliyoko katika Yuda na Benyamini, miji yenye maboma.

11. Akazifanya imara hizo ngome, akaweka majemadari humo, na akiba ya vyakula, na mafuta, na mvinyo.

12. Na ndani ya miji yote mmoja mmoja aliweka ngao na mikuki, akaifanya kuwa na nguvu nyingi mno. Yuda na Benyamini ikawa milki yake.

13. Wakamwendea makuhani na Walawi waliokuwa katika Israeli yote, kutoka mpaka wao wote.

14. Kwani Walawi wakaacha malisho yao, na milki yao, wakaja Yuda na Yerusalemu; kwa sababu Yeroboamu na wanawe waliwatupa, ili wasimfanyie BWANA ukuhani;

15. naye akajiwekea makuhani wa mahali pa juu, na wa wale majini, na wa zile ndama alizozifanya.

2 Nya. 11