2 Kor. 13:7-10 Swahili Union Version (SUV)

7. Nasi twamwomba Mungu, msifanye lo lote lililo baya; si kwamba sisi tuonekane tumekubaliwa, lakini ninyi mfanye lile lililo jema, tujapokuwa sisi tu kama waliokataliwa.

8. Maana hatuwezi kutenda neno lo lote kinyume cha kweli, bali kwa ajili ya kweli.

9. Maana twafurahi, iwapo sisi tu dhaifu, nanyi mmekuwa hodari. Tena twaomba hili nalo, kutimilika kwenu.

10. Kwa sababu hiyo, naandika haya nisipokuwapo, ili, nikiwapo, nisiutumie ukali kwa kadiri ya uwezo ule niliopewa na Bwana, kwa kujenga wala si kwa kubomoa.

2 Kor. 13